Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masood Melimeli akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama akipatiwa matibabu baada ya kukatwa mapanga |
Mtendaji wa Kata ya Ubagwe Stephen Kimario aliyepigwa vibaya sehemu na kichwani |
Kampeni za uchaguzi mdogo wa Kiti cha Udiwani katika
kata Ubagwe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga umeingia dosari baada ya watu
wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendele (CHADEMA)
kuvamia na kuwajeruhi vibaya wafuasi wa CCM kwa kuwajeruhi vibaya kwa kuwakata
mapanga.
Akiongea katika Hspitali ya Wilaya ya Kahama
alipolazwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masood Melimeli alisema kuwa
tukio hilo lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku wakati wafuasi hao wa
chama hicho wakitokea katika kijiji cha Ihata kwenda kwenda Itobola katika
Kampeni.
Alisema kuwa walipofika katikakati ya Pori
walikutana na gari ya CHADEMA aina ya Toyota land Cruser ikiongozwa na Mbunge
wa Jimbo la Maswa Masahariki Sylivesta Kasulumbai na kuanza kuwashambulia kwa
kutumia mapanga, Nondo pamoja na fimbo na kuwajeruhi vibaya watu sita akiwemo dereva wa gari za
CCM huku wengine wawili wakipotea kusikojulikana.
Waliojeruhiwa katika mapambano hayo ni pmaoja na
Katibu Mwenezi wa CCM Masood Melimeli aliyeimia sehemu ya mkono na Bega,
Ramadhani Salumu aliyepigwa panga la Mguu na Mkono, Sebastian Masonga
aliyevunjwa Mkono wa kushoto, Dereva Charles Muhiga aliyejeruhiwa sehemu za
kichwani, Mtendaji wa Kata ya Ubagwe Stephen Kimario aliyepigwa vibaya sehemu
na kichwani na kupasuka na hali yake ni mbaya.
Melimeli alisema kuwa katika tukio hilo wafuasi
wawili wa Chama hicho waliofahamaika kwa jina moja moja na Ismail na Samweli
wao walipotea kusikojulikana na kutokana na kuona wenzao wakishambuliwa vibaya
kwa kutumia vitu vyenye ncha kali vikiwemo Nondo pamoja na mapanga.
Kwa upande wake katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa
Shinyanga Emanuel Mlimandago amelaani kitendo hicho na kusema kuwa hiyo siyo
demokrasia ya kweli na kuongeza kuwa Watanzania wote hawanabudi kukilaani.
Katika vurugu hizo ambazo zinasadikiwa kufanywa na
wafuasi wa Chadema, Mbunge wa Jimbo la Maswa mashariki Sylivesta kasulumbai anashikiliwa
na jeshi la Polisi Wilaya ya Kahama kwa mahojiano zaidi kuhusu kufanyika kwa
tukio hilo.
Nae Mwenyekiti wa TADEA Wilaya ya Kahama Charles
Lubala akizungumzia kuhusu tuki hilo alisema kuwa mfuasi wa CHADEMA alivamia
katika mkutano wa CCM na ndipo walipomkamata na kumuweka katika gari la CCM kwa
lengo la kumpeleka katika kituo kidogo cha Polisi Bulungwa.
Hata hivyo baada ya kumuweka katika gari la CCM
wafuasi wa chadema walipotangulia mbele na kuweka vizuizi barabarani na hivyo
kusababisha vita hivyo kufanyika na kupelekea watu haoa sita kujeruhiwa huku
hali ya Mtendaji wa kata hiyo ikiwa ni mbaya na amelazwa katika Hospitali ya
Wilaya.
“Kwa kweli hizi kampeni zimekuwa kama vita kwa sasa ni hatari na unapaswa kujihami
kikamilifu kwani unaweza kupoteza maisha hivi hivi kwa ajili ya Kampeni hizi
zinazoendelea hapa Ubagwe”, Alisema Mwenyekiti huyo wa TADEA Charle Lubala.
Hata hivyo katika kuonyesha kuwa kunaweza kutokea
vurugu katika kata hiyo ambayo uchaguzi wake wa udiwani unatarajiwa kufanyika
tarehe tisa mwezi huu vijana wa CCM walionekana kujiandaa vilivyo baada ya
kuondoka kwenda katika kampeni hizo huku baadhi yao wakiwa wamesheni majambia.
Kampeni za Uchaguzi katika kata ya Ubagwe Wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga zinafanyika kufuatia aliyekuwa Diwani katika kata hiyo
Richard Mndula kufariki Dunia mwaka jana huku kinyang’anyiro hicho
kikiwahusisha wagombea watatu kutoka
katika vyama vitatu vya CCM, TADEA
pamoja na CHADEMA.
No comments:
Post a Comment