Friday, February 14, 2014

MAPANGA YA YA CCM NA CHADEMA YATIA HOFU WALIMU KATIKA USIMAMIZI



Na Raymond Mihayo
Kahama
Febr 14, 2014.

UKATANAJI WA MAPANGA KATIKA MAMBO YA UCHAGUZI YAWATIA HOFU WALIMU KAHAMA

KUFUATIA hali ya vurugu ya kukatana Mapanga kwa Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wale wa CCM  iliyojitokeza katika Kampeni za uchaguzi Mdogo wa kiti cha udiwani katika kata ya Ubagwe Wilayani Kahama Mkaoni Shinyanga imewatia wasiwasi Walimu katika kusimamia uchaguzi Uchaguzi Mkuu ujao.

Wasiwasi huo ulitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Shinyanga George Nyangusu katika kikao cha Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kahama kilichofanyika mjini hapa na kujumuisha wanachama wake wa Wilaya za Ushetu, Kahama Mjini na Msalala.

Katika Mkutano huo ambao ulijumuisha zaidi ya Walimu 333, Mwenyekiti huyo alisema kuwa vitendo vilivyofanywa na wafuasi wa vyama hivyo viwili imeleta sura mpya kwa Walimu amba kwa kiasi kikubwa ndio wasimamizi wa chaguzi mbalimbali zinazoendeshwa ba Serikali.

“Sisi Walimu hali hiyo mpaka kufikia sasa inatutisha katika zoezi zima za kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao kutokana na vitendo vya ukataji wa mapanga yaliotokea hasa katika kata ya Ubagwe na kwa huili serikali iliangalie kwa umakini lisijirudie tena”, Alisema George Nyangusu.

Aidha Nyangusu alisema kuwa inasikitisha kwa Wilaya ya Kahama yenye rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na misutu kuona katika shule zake za msingi bado kuna kundi kubwa la Wanafunzi wanaofundishwa wakiwa wamekaa chinina kuongeza kuwa hali hiyo ni hatari kwa taifa la kesho.

Akisoma Risala ya Chama hicho Katibu wa Chama cha Walimu Wilaya ya  Kahama
Simon Keha alisema kuwa Walimu wanakabiliwa na Changamoto nyingi katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa ratiba za ukamilishaji za masomo ambapo wanafunzi wanatoka muda wa saa 12 tofauti na maeneo mengine.

Keha aliendelea kusema kuwa Changamoto nyingine ni pamoja na lugha mbaya zinazotolewa  kutoka kwa Watendaji wa Serikali  ikiwa sambamba na kucheleweshewa madai mbambali wanayokuwa wakidai kama fedha za uhamisho katika Halmashauri husika.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Frolence Mpeta alisema kuwa Serikali inamtemea Mwalimu katika masuala mbalimbali  ikiwa sambamba nay ale ya Uchaguzi Mkuu.

Mpeta alisema kuwa Suala la Walimu kupewa fedha za uhamisho kwebnda katika kituo kingine lipo ndani ya uwezo wao na kuongeza kuwa atahakikisha kuwa masuala hayo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo kwani kwa kufanya hivyo hivyo kunaweza kuwapa Walimu morali ya kufanya kazi.

  

No comments:

Post a Comment