Na
Raymond Mihayo
Kahama
Febr
28,2014.
WATENDAJI
WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI WATAKIWA KUTOKAA MOFISINI
WATENDAJI
wa Waizara ya Niashati na Madini waliopewa Dhamana ya kusimamia sheria za
Wachimbaji wadogo hapa Nchini wametakiwa kutokaa maofisini badala yake
wazunguke kwa wachimbaji wadogo kwa
madhumuni ya kutoa Elimu kwao juu uchimbaji wa kufuata sheria.
Hayo
yalisemwa juzi na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo Mkoa wa
Shinyanga Nicodemus Majambe wakati akiongea na Mwandishi wa habari hizi juu ya
vikwazo wanavyovipata Wachimbaji wadogo hapa nchini katika kupata maeneo ya
Uchimbaji.
Majabe
alisma kuwa Wachimnbaji wadogo hawana Elimu juu ya kupata maeneo ya uchimbaji
wa Madini na kuongeza kuwa kama maafisa wa Madini wasingekaaa maofisini basi
kusingekuwa na migogoro yeyote juu ya kupata maeneo ya Uchimbaji.
Alisema
kuwa katika meneo ya Uchimbaji wa Madini Wakuu wa Wilaya wamekuwa wakipta kazi
ya kutoaa Elimu ya uchimbaji katika maeneo hayo kazi ambayo ilitakiwa kutolewa
na maafisa wa Madini wa Sehemu husika.
Makamu
Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika Mkutano waliokaa na Waziri wa Niashati na
Madini Mjini Dodoma walikubali kuwa na ushirikiano mkubwa baina ya Wachimbaji
wadogo na uongozi wa Wizara ya madini kwa ujumla.
Pia
alisema kuwa urasilimu ulipo kati ya Watendaji wa Wizara ya Madini na Nishati
Tanzania ndio unaosababisha kuwepo migogoro mingi baina ya Wachimbaji wadogo na
Wizara ya Madini na Nishati Hapa nchini.
“Kuna
kesi nyingi ambazo zipo baina ya
Wachimbaji wadogo na Maafisa Madani katika Wilaya mablaimbali hapa nchini
lakini Wizara husika inakuwa haina taarifa juu yakuwepo kwa Migogoro hiyo hali
inaleta mvutano mkubwa baina yapande hizo mbili”, Alisema Nicodemus Majabe.
Aidha
alisema kuwa baadhi ya migogoro hiyo ni pale wachimbaji wadogo wanapoomba leseni
za maeneo ya kuchimba lakini wamekuwa
wakipewa maeneo tofauti na y ale waliomba huku yale ya awali wakipewa
wawekezaji wenye uwezo.
Makamu
Mwenyekiti huyo alimuomba Naibu Waziri anayehusika na kitengo cha Madini
Stephen Masele kujitahidi katika kuondoa migogoro hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa
imekuwa ni kero kwa Wachimbaji wadogo na Wawekezaji wa migodi.
mwisho
No comments:
Post a Comment