Na Raymond Mihayo
Kahama
March 23/ 2014.
WAKANDARASI WATAKIWA KUMALIZA KAZI ZA MIRADI YA MAJI
KWA WAKATI
SERIKALI imewataka Wakandarasi wanaojenga miradi
mbalimbali ya maji Mkoani Shinyanga
wametakiwa kumaliza kazi za miradi hiyo waliopewa na Halmashauri husika kwa wakati kwa mujibu wa mikataba yao ya kazi
inavyoonyesha kumaliza kazi hiyo.
Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Ally Rufunga katika kilele cha Wiki ya maji ambayo ambao kimkoa ilifanyika
katika kijiji cha Kagongwa Wilayani Kahama na kusisitiza kuwa wakandarasi wengi
wamekuwa wakikwamisha miradi hiyo.
Rufunga alisema kuwa kama Wakandarasi wangekuwa
wakimaliza kazi mapema ya kujenga miradi ya maji basi Wananchi wangeweza
kufaidika na michango yao ambao wamekuwa wakichanga katika kufanikisha huduma
hiyo muhimu.
Pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga aliwataka
wananchi wanapopata miradi ya maji katika maeneo yao kujitahidi kuiunga mkono
Serikali kwa kutoa ushirkiano katika suala zima la kuchangia miradi hiyo ili
iweze kuwanufaisha watu wa maeneo hayo hasa maeneo ya Vijijini.
Aidha katika kilele hicho cha Wiki ya maji Mkuu huyo
wa Mkoa wa Shinyanga alifungua mradi wa maji wa Kagongwa Iponya uliosimamiwa na
Halmashauri ya Wilaya ya Kahama wenye thamani ya shilingi milioni 432.4 ambao
utahudumia jumla ya wakazi 11,293 wa vijiji hivyo pamoja na Tanki lenye uwezo
wa kuchukua lita zipatazo 50,000 za maji.
Rufunga alisema kuwa kupata maji kwa wakazi wa
Kagongwa na Iponya Wilayani Kahama kuwa ni mwanzo tuu wakisubiri mradi mkubwa
kule wa ziwa ziwa Victoria ambao utapita katika Kata hiyo ukipeleka maji katika
maeneo ya Isaka, Tinde mpaka Tabora ambao upo katika upembuzi yakinifu kwa sasa
ukisubiri bajeti ijayo kwa ajili ya
kuanza kwa ujenzi wa mradi huo.
Awali akisoma Risala kwa naiba ya Halmashauri ya
Wilaya Mhandishi Charles Pambe alisema kuwa mpaka kufikia hivi sasa nia
asilimia 63 ya Wakazi wa Halmashauri ya mji wa Kahama ndio wanaopata huduma ya
maji safi na salama na kuongeza kuwa kiwango hicho bado ni kidogo kulinganishwa
na kile cha Taifa.
Pambe alisema kuwa kwa upande wa Changamoto
zinazikabili Idara yake ya maji katika Mji wa Kahama na pamoja maeneo ya
Vijijini kitendo cha Wananchi kutoshiriki katika kuchangia huduma za maji hali
ambayo inafanya sehemu nyingi za Vijijini kutokuwa na maji kwa muda mrefu.
mwisho
No comments:
Post a Comment