Na Raymond Mihayo
Kahama
March 7, 2014.
SERIKALI imeshauriwa kuweka mfuko maalum kwa ajili
ya kuendeleza Kilimo cha Pamba hapa nchini badala ya kupoteza fedha zake nyingi
katika kendesha vikao vinavyohusu zao hilo.
Ombi hilo lilitolewa juzi na Meneja wa Kiwanda cha
Kahama oil Mil Wiliam Matonange wakati akizungumza na waandishi wa habari juu
Kilimo cha mkataba ambacho wao kama wanunuzi wa zao hilo hawakubaliani nacho.
Matonange alisema kuwa Wakulima kwa sasa wanakuwa na
wakati Mgumu wa kulima zao hilo kutokana na kuwa hawana dhamana na kuweka
katika makampuni ya ununuzi wa zao hilo ili waweze kukopesheka.
Aidha Meneja huyo aliendelea kusema wao kama
makampuni ya ununuzi wa zao hilo wanashindwa kuwakopesha wakulima hao na
kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo ni lazima kufunga nao mkataba.
“Ukifanya kilimo cha Mkataba na Wakulima ni sawa na
kujitia hasara kwani Wakulima wanachotegea ni hali ya hewa ya wakati huo hali
ambayo kama mvua ikikataa kunyesha itakuwa hasara kwa Kampuni”, Alisema Matonge
Akizungumzia kuhusu kukamatwa na kuwekwa ndani kwa
kutuhumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Magalula kuwa makampuni hayo
yamekuwa yakiwaibia wakulima Meneja alisema kuwa madai yake sii ya kweli.
Ilidaiwa mkutano wa Wanunuzi wa zao la Pamba
uliofanyika Mkoani Geita kuwa baadhi ya Makampuni yaliokopeshwa mbegu na
viwadudu na Bodi ya Pamba kwa nia ya kuwakopesha wakulima hawakufanya hivyo
badala yake waliwauzia wakulima hao kwa
asilimia mia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula
Magalula alisema kuwa kuna baadhi ya Makampuni yaliopewa mbegu hizo na Viwadudu
hayakuwakapopesha wakulima kama
walivyokubaliana katika kikao husika.
Magalula aliendelea kusema kuwa kuna baadhi ya
Mawakala ambao pia ni wanunuzi wa zao la
Pamba walifanya kinyume na makubaliano ikiwemo Kampuni ya Kahama oil mil.
MWISHO
No comments:
Post a Comment