Kahama
March 9, 2014.
WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA UZAZI
WA MPANGO
AKINAMAMA Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
wametakiwa kujitokeza katika kupata Elimu ya uzazi wa mpango kwalengo la kuzaa watoto wachache wanaolingana na mahitaji
ya familia wanazoishi ikiwa ni pamoja na kumudu gharama za kuwasomesha.
Hayo yalisemwa juzi na Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali
ya Wilaya ya Kahama Emeleciana Machibya wakati akipokea msaada wa vifaa
mbalimbali kutoka kwa Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa Buzwagi katika
sherehe za siku ya Wanawake Duniani.
Machibya alisema kuwa kwa jamii ya Kabila ya
Wasukuma kwa kila kaya ina wastani wa kuzaa watoto nane na kuendelea hali
ambayo inakuwa vigumu katika suala zima la kuwalea watoto hao pamoja na kuwapa
Elimu.
Alisema kuwa katika usiku wa kuadhimisha siku ya
Wanawake Duniani jumla ya watoto 20 walizaliwa katika Hospitali idadi ambayo
alisema kuwa ni ya kiwango cha juu kuliko hata Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga
ambayo ina idadi ndogo.
Katika kuadhimisha siku hiyo ya Wanawake Wilayani
Kahama Wanawake hao wanafanaya kazi katika Mgodi wa Buzwagi wakiongozwa afisa
Mahusiano wa Mgodi huo Salome Makamba walitembelea katika Hospitali ya Wilaya
ya Kahama na kutoa msaada vitu mbalimbali katika wodi ya wazazi kama vile
Sabuni, Mabeseni, Kanga pamoja na vitu vingine vyenye thamani ya shilingi
milioni 1.7.
Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi
Salome Makamba alisema kuwa wao kama Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi huo
waliamua kujichangia fedha kwa ajili ya kusaidia wazazi hao ambao wengi wao ni
wanawake wanaishi Vijijini wasiokuwa na uwezo.
Pia Makambali alishauru Wanawake wengine wenye
mapenzi mema kujitokea katika kuwasaidia wazazi katika Hospitali hiyo kwani
kutoa ni moyo na wala sio utajiri na kuongeza Kampuni hiyo ya Africna Barrick itakuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha akinamama wanasonga mbele.
Nae Mmoja wa Wanawake walioambatana katika msafara
huo Mwajuma Ramadhani akiongea na Wanafunzi wa kike wa Shule ya sekondari ya
Mwendakulima aliwataka wanawake kujiamini na kujiona kuwa wanaweza kufanya
chochote na kuacha kuwa na tama na kuridhika na kila kitu wanachikipata.
Katika siku hiyo ya Wanawake Duniani Wafanyakazi hao
wa Kike kutoka katika Mgodi wa African Barrick gold Mine inayomiliki Mgodi wa
Buzwagi walitoa msaada huo kwa akinamama 45 na watoto 40 katika Hospitali hiyo
pamoja na Madaftari kwa Wanafunzi wa kike 50 wa Shule ya sekondari ya
Mwendakulima mjini Kahama.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment