Na Raymond Mihayo
March 16,2014
Kahama.
NANE WAFARIKI DUNIA BAADA YA
KUANGUKIWA NA VIFUSI WAKICHIMBA DHAHABU KAHAMA
WATU 8 wamefariki Dunia na moja kunusurika katika
machimbo Madogo ya dhahabu katika
kijiji cha kalole na Nyangalaya kata ya lunguya
wilayani kahama mkoani shinyanga baada ya kuangukiwa na vifusi katika mashimo
waliokuwa wakichimba.
Akiongea na Waandishi wa Habari juu
ya tukio hilo Mtendaji wa kijiji cha kalole Furaha mashamba ,alisema kuwa watu
saba walikufa katika machimbo ya Kalole huku mmoja akifariki katika machimbo ya
Nyangalata na hivyo kufikia idadi hiyo.
Mashamba alisema kuwa matukio hayo
yalitokea juzi juzi majira ya saa 5
usiku ambapo wachimbaji hao wadogo katika
machimbo hayo walifukiwa na udongo wa dhahabu katika mashimo walikuwa
wakichimba.
Afisa Mtendaji huyo wa kijiji alizidi
kusema kuwa wanakijiji hao katika
matukio hayo waliweza walishirikiana ili kuweza kuwaokoa wachimbaji hao hao
baada ya tukio lakini ilishindikana na hivyo kufanikiwa kutoa miili saba na
moja akiwa hai na kukimbizwa kituo cha Afya Lunguya kwa matibabu zaidi .
Adhia mtendaji huyo
aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Mandogo Kibasi Kiaka (26) msukuma
mkazi wa kalole ,Juma Malingaya miaka( 30) msukuma mkazi wa kalole ,Charles
Iheyolo miaka (21)msukuma mkazi wa kalole ,Roma Masolwa miaka( 26)msukama mkazi
wa kalole ,Juma John miaka( 33)msukuma mkazi wa kalole ,Paul Jemes miaka (24)
msukuma mkazi wa kalole ,Ngaleba Kacheyekele miaka (24) na Michael Pius miaka
(43)mkazi wa morogoro kabila mpongolo ambaye alinusurika,
Akifafanua zaidi Mtendaji alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa ni
mashimo hayo kutokuwa na usalama wa kutosha na kuingiliwa na maji chini ya
mashimo hayo kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha Wilayani hapa .
Aidha Mtendaji Furaha alisema kuwa maeneo haya yalishapigwa
marufuku lakini wamekuwa wakiyavamia mara kwa mara hilo na kuongeza kuwa suala
hilo limekiwa ni tatizo sana kwa
wachimbaji wadogo wadogo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kwa upande wake Mjiolojia wa Madini wilayani kahama Amir Chande alisema kuwa maeneo haya katika
kijiji cha kalole walishayafunga kutokana na maeno haya kuwa ni hatari kwa usalama
wa wachimbaji na wamekuwa wakinyavamia
mara kwa mara na kusababisha vifo vya mara kwa mara.
“Kuanzia sasa ni marufuku kwa Wachimbaji kuchimba katika maeneo
hayo hadi hapo Serikali itakapotoa maelekezo juu ya ni maeneo gani wanayotakiwa
Wachimbaji wadogokuchimba kwa usalama wao na kufuata sheria na taratibu za
uchimbaji’,Alisema Jiolojia huyo.
“ hapa nyinyi mpo kimakosa na kwa sababu hakuna mwenye leseni
hapa ya uchimbaji wa madini kwa hiyo sasa ni makosa kufanya kazi hii ya
uchimbaji na kuanzia sasa machimbo tunayafunga kwa usalama wenu”, Alisema chande ”
Aidha afisa huyo alizidi kufafanua
kuwa ofisi yetu ipo wazi kwa kila mtu anayeteka leseni ya uchimbaji na siyo
kuvamia maeneo ya makampuni nyenye
leseni na kuongeza kuwa mtu kuomba leseni ya uchimbaji wa madini
mahali popote hapa Tanzania kwa maeneo ambayo tayari yana leseni za watu .
Mwisho
No comments:
Post a Comment