Wednesday, June 4, 2014

MALIPO YA MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU KWA SERIKALI NI KIASI CHA SHILINGI BILIONI 111.3 KWA MWAKA 2010/2011.


IMEELEZWA kuwa katika Ripoti ya Tatu ya Mpango wa Uhamasishaji  uwazi katika mapato ya Madini , gesi Asilia  na  Mafuta ( TEITI) kwa mwaka 2010/ 2013 inaonyesha kuwa  Malipo yaliopokelewa na Serikali kutoka katika Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi na jumla ya shilingi Bilioni 111.3.

Hayo yalisemwa juzi na katibu Tawala Wilaya ya Kahama Julius  Mushi wakati akifungua warsha ya siku moja kwa ajili ya kuelimisha umma kuhusu Ripoti ya tatu ya TEITI yenye malipo na mapato ya madini na Gesi asilia  katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011.

Warsha hiyo pia ailiwajumuisha Viongozi mbalimbali kutoka katika sehemu zinzochimbw madini pamoja na Asasi za Kiserikali katika maeneo ya Mwime, Zongomela, Kakola, Nyangala pamoja na maeneo mengine mengi.

Katibu Tawala huyo alisema kuwa idadi hiyo ya fedha kinahusisha  kodo zote na Mrabaha na kuongeza kuwa pia Halmashauri zilizopo katika maeneo husika katika migidi hiyo yalifaidika kwa kupata kiasi cha Dolla  za kimarekani 200,000 sawa na shilingi milioni 250 kwa kila Halmashuri husika.

Mushi aliendelea kusema kuwa kwa uwazi huo kwa wawekezaji hao kuwa wazi ni haki kwa kila Mwananchi kujua matumizi ya fedha hizo  kama zinatosheleza au nini kifanyike juu ya fedha hizo zinaotlewa na wawekezaji walipo katika eneo la Halmashauri husika.

Katibu Tawala huyo aliendelea kusema kuwa pia pamekuwepo na kutoridhika kwa tozo ambayo Halmashauri za Wilaya zenye migodi ya Madini  zimekuwa ziklipwa na makapuni ya madiini takribani dolla za kimarekani 200,000 kila Halmashauri bila ya kujali ukubwa wa shughuli za Kampuni husika .

Alisema kuwa Migodi imekuwa ikichangia kwa hiari katika kuimarisha huduma za kijamii  pamoja na kuchangia Elimu na Miradi mingine ya kimaendeleo katika jamii inayozunguka migodi hiyona kuongeza kuwa michango hiyo imekuwa wazi katika ripoti ya pili nay a tatu ya TEITI.

Hata hivyo Katibu Tawala huyo wa Wilaya ya Kahama aliendelea kusema Wananchi pia Wanapaswa kujua na Michango ya kampuni husika katika ngazi za uamuzi wa aina ya miradi wanayotaka ichangiwe na Kampuni husika.

Alisema kuwa Tanzania imeanza kuona matunda ya kujiunga na TEITI kutokana na tofauti zinazojitokeza kati ya kodi  zinazolipwa na Kampuni na mapato yaliopokelewa na Serikali  imekuwa ikipungua na kuongeza kuwa uchunguzi wa tofauti hizi unafanywa na mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.



No comments:

Post a Comment