Juni 27, 2014.
WATUMISHI WA MAHAKAMA KAHAMA NA BUKOMBE WAPIGWA
MSASA.
WATUMISHI wa Idara za Mahakama wakiwemo Mahakimu na
Makarani wa Wilaya za Bukombe na Kahama
juzi wamepata mafunzo ya kutoka katika mfumo wa karatasi kwenda katika mfumo
kwa Kopyuta (JSBS) kwa lengo la kukuza ufanisi katika maeneo yao ya kazi
waliopo.
Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika Mjini Kahama
yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao wa kufanya kazi kutoka
katika mfumo huo wa zamani wa karatasi kwenda katika mfumo wa Kopyuta unaotumiwa
na taasisi nyingi kwa sasa hapa duniani.
Mwezeshaji wa Semina hiyo kutoka idara ya Mahakama
makao Makuu Samweli Fredrick alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kupata ripoti
kwa urahisi kutoka watumishi hao kuliko ilivyokuwa hapo awali walipokuwa
wakitumia mfumo wa karatasi.
Fredrick alisema kuwa mfumo wa karatasi uliokuwepo
awali kuwa ukiwawia vigumu kupata taarifa kwa haraka pindi zinapotakiwa kwa
kuwa watumishi hao walikuwa wakitumia mfumo wa zamani wa kutumia karatasi hali
ambayo ilikuwa inachukua muda mrefu.
Alisema kuwa kwa kutumia mfumo mpya huu wa Kopyuta
itaweza kuwasadia kupata taarifa kwa haraka kwa kila mahakama hapa nchini pindi
zinapotakiwa na msajili wa Mahamakama hapa nchini au viongozi wengine wa ngazi
za juu hapa nchini.
Kwa upande wake Mratibu wa Semina hiyo Gadiel Marick
alisema kuwa semina hiyo imewashirikisha washiriki 32 kutoka katika Wilaya za
Bukombe na Kahama na kuongeza kuwa mafunzo hayo yanatarajia kuleta mabadiliko
makubwa ya utendaji wa kazi katika idara ya mahakama
Aidha Mratibu huyo aliendelea kusema kuwa Watumishi
wa Mahakama awali wengi wao walikuwa hawajui mfumo wa kutumia Kopyuta hali
ambayo kwa kupata mafunzo hayo hayo itakuwa ni chachu kwao katika utendaji wa
kazi wao kwa kutumia mfumo huo mpya katika idara ya Mahakama hususani katika
Wilaya hizo.
Marick alisema kuwa huu ni muda muafaka kwa
Watumishi hao kupata mafunzo hayo hasa ukizingatia Wilaya za Bukombe na Kahama
zimekuwa na mrundikano wa Matukio mengi ambapo kesi zilizopo Mahakamani nyingi
na kuongeza kuwa kwa mafunzo mafunzo yanaweza kuwa ni moja sehemu ya kupunguza
kesi zilizopo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment