Na Raymond Mihayo.
KUENDESHA Biashara bila ya kufuata misingi ya
Sheria, taratibu na kiwango cha juu cha maadili ni moja kati ya Changamoto zinazowakabili
Wafanyabiashara Mkoani Shinyanga kupata fursa ya kufanya biashara na Migodi ya
Barrick Tanzania.
Kutokana na kupungukiwa kwa vigezo hivyo
kumesababisha Wafanyabiashara hao kukosa fura za kuomba zabuni katika migodi
hiyo hali ambayo imefanya wale walipo nje ya Mkoa wa Shinyanga kupata fursa
hizo.
Pia tumezoea kuona jamii iliyopo karibi na
Wawekezaji wa aina yoyote ikifadika kutoka na rasilimali zilizopo katika eneo
husika lakini kwa Wafanyabiashara walipo katika Mkoa wa Shinyanga hususani
katika Wilaya ya Kahama wakikosa fursa hizo.
Ukiangalia sababu muhimu za kukosa kuchangamkia
fursa hizo ikiwa ni pamoja na kufanya biashara na Mwekezaji huo ni pamoja na
kuwa Elimu duni, bidhaa zisizokuwa na kiwango pamoja na kufuata maadili
biashara.
Kwa hali hiyo imekuwa ni kazi kubwa kwa
Wafanyabiashara walipo katika Mkoa wa Shinyanga kupata fursa hiyo ikiwa ni
sambamba na kutoungana kwa pamoja na kuwa na mitaji mikubwa kwa ajili kupata
fursa za kupata nafasi ya kufanya biashara na migodi hiyo.
Tangu kufunguliwa kwa migodi hiyo ya Barrick ya
Bulyanhulu na Buzwagi ni Wafanyabiashara kutoka nje ya Mkoa wa Shinyanga
wamekuwa wakipata nafasi ya kufanya biashara na migodi hali ambayo ni
changamoto kwa wale waliopo katika maeneo husika ya Migodi ilipo.
Katika migodi hiyo kuna fursa nyingi za kibiashara
kama vile za mayai, Nyama, Mboga za majani
na hata matunda lakini kwa kutokuwa na mitaji mikubwa ya kuendeshea
biashara hizo imekuwa ni vigumu kupata fursa katika migodi miwili na hivyo kuwaacha
wale wan je ya Mkoa wa Shinyaga wakineemeka.
Kutoka na sababu hizo Kampuni ya Barrick Bulyanhulu na ile ya
Buzwagi iliamua kuendesha Mkutano wa siku moja mjini Shinyanga kwa ajili ya kutoa Elimu ya kufanya biashara na
Migodi hiyo kwa lengo la kuwapatia fursa
ya kufanya biashara na migodi hiyo iliyopo katika Mkoa wa Shinyanga.
Hapo awali kulikuwa na malalamiko ya juu ya Migodi
hiyo kuwa ilikuwa ilkielekeza nguvu kubwa katika kuwapatia nafasi
Wafanyabishara kutoka nje ya Mkoa wa Shinyanga kufanya nao biashara za manunuzi
huku wale wa ndani wakisahaulika.
Kati ya malalamiko hayo ni pamoja na na zile
biashara nadogo kama za matunda, na hata mbogamboga ambazo wale Wafanyabiashara
waliopo katika eneo husika wamekuwa wakikosa nafasi hizo hali ambayo ilizua
malalamiko miongoni mwao.
Filbert Rweyemamu ni Meneja Mgodi wa Barrick Buzwagi
akizungumzia kuhusu suala hilo anasema kuwa wanafanya ununuzi wa ndani kwanza
kwa kuzingatia thamani bora kila iwezekanapo na kuongeza kuwa huo ni mpango endelevu wa
Kampuni.
Rweyemamu anasema kuwa kanuni za ushindani bora wa
kibiashara unajumuisha gharama pamoja na jumla ya bidhaa pamoja na mtazamo wa
pamoja katika suala zima la kiusalama , Afya na mazingira yalipo katika Mgodi
huo.
Anasema kuwa faida za ununuzi wa ndani wa jamii inayozunguka mgodi ni kushirikiana
na Wafanyabishara wa ndani kuendeleza uchumi wa ndani ya nchi na eneo husika
uliopo mgodi husika pamoja na kutoa fursa katika ngazi ya jamii za katika
kujishughulisha katika masuala ya kibiashara.
Pia anasema kuwa lengo jingine ni kuongeza fursa za
ajira na kuongeza ubora wa bidhaa zinazopatikana hapa nchini na kuongeza ufanisi wa wagavi wa ndani ili
kuongeza pato la Serikali kupitia kodi mbalimbali.
Anasema kuwa faida zinazopatikana katika ununuzi wa
ndani kwa Kampuni ni pamoja na kupunguza
thamani ya bidhaa zinazoifadhiwa kwa wingi na kuongeza mzunguko wa fedha katika
kufanya uwekezaji kwenye miradi mingine.
Aidha anasema kuwa pia ni kuounguza muda wa kuagiza
na kusafirisha bidhaa kutoka nje ya Mkoa wa Shinyanga pamoja na nje ya
nchi na kuongeza kuwa hii inasaidia kuwa
raia Mwema katika jamii inayowazunguka katika Kampuni yake.
Anasema kuwa changamoto zinazowakabili
Wafanyabishara wazalendo ni kuonyesha
uwezo wao kwenye kipimo cha (PQQT) ikiwa
na maana bei za ushindani ni za juu
kuliko bei za nje ikiwa sambamba na
ushuru na usafiri.
Anasema kuwa ubora wa bidhaa au huduma, Idadi
inayohitajika, pamoja na muda wa
kuchukua kutoka kupata PO hadi kufikisha
kwenye Kampuni ya Afican Barrick Gold
Mine.
Rweyemamu anasema kuwa kushindwa kutoa majibu ya
haraka kuhusu bei na upatikanaji wa
bidhaa pamoja na ka kutoweza kutoa mawasiliano ikiwa kuna matatizo au
uchelewaji ambao haukutarajiwa nayo pia
imekuwa tatizo kubwa.
Meneja Mkuu huyo wa Mgodi wa buzwagi anabainisha
sababu au changamoto inaowakabili wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga kuwa ni
pamoja na kuendesha Biashara zao bila ya kufuata misingi ya kisheria ,
taratibu na kiwango cha juu cha maadili.
Anasema kuwa pia hakuna ushirikiano baina yao na kuwa na ushindani usiokuwa na mtazamo wa
kibiashara na kukataa kuungano ili
kupata kazi kubwa ya kufanya katika Kampuni hizo za Barrick Buzwagi na ile ya
Bulyanhulu na pia Wafanyabiashara kuridhika na kutotaka kujiendeleza .
Anasema kuwa Usajili wa madaraja ya chini kwa Wakandarasi, kuondesha biashara zsao kwa
majina yao binafsi na usalama juu ya
taratibu za kazi na uzalishaji na utunzaji mazingira pia moja ya changamoto
kubwa zinazowabaili wafanyabiashara kutoka Mkoa wa Shinyanga.
Anasema kuwa Mpango ulionao Kampuni za Barrick kwa
sasa za kuondeleza Ugavi wa ndani ni
kuongeza ukubwa wa biashara inayofanyika ,ukongeza idadi ya bidhaa na huduma
zinazonunuliwa katika maeneo husika au
yote hapa nchini.
Pia kuwajengea uwezo ili waweze kufikia viwango
vinavyotakiwa na Afican Barrick kwa muda maalumu na kuangali taratibu
zinazoweza kufikiwa kirahisi na wagavi wazalendo bila ya kuathiri taratibu za Afican Barrick
Gold Mine.
Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Ally Rufunga akifungua mkutano huo uliandaliwa na Kampuni ya
African Barrick Gold Mine anasema kuwa Wafanyabiashara hasa wa Mkoa wa Shinyanga
wanapaswa kujua kuwa wao bado wana fursa kubwa ya kufanya kazi na migodi hiyo
miwili.
Anasema kuwa anawashukuru pia Uongozi wa Migodi hiyo
miwili ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa kufanya mkutano na kutoa Elimu kwa
Wafanyabiashara hasa wa Mkoa wa Shinyanga katika kufuata Sheria na muda katika
kuendesha biashara zao hasa katika maeneo ya wawekezaji wa Migodi.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga anasema kuwa
Wawekezaji wanataka bidhaa zenye kiwango na kuongeza kuwa kwa kutumia Mkutano
huo Wafanyabiashara wa Mkoa waShinyanga hawana budi kubadilika na kuongeza kuwa
kama kuna masuala ya kiserikali yanayowasumbua basi ofisi yake ipo wazi kwa
kutoa kutoa ushauri wa kibishara.
Pia Rufunga anawaomba Kampuni hiyo kuwa na utaratibu
wa kuendesha mikutano kama hiyo mara kwa mara kwa lengo la kutoa Elimu kwa
Wafanyabiashara hao hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko hasa kwa
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga kuweza kuchangamkia fursa zilizopo katika
migodi inayowazunguka.
Mkutano huo wa siku moja uliofanyika mjini Shinyanga
ulijumuisha Wafanyabiashara kutoka Mkoa wa Shinyanga na wale ambao tayari
walishaanza kufanya biashara na kampuni hiyo huku lengo kubwa likiwa ni kutoa
Elimu kuhusu kuweza kupata fursa za kufanya biashara na Kampuni ya Barrick.
Nao Wafanyabiashara waliohudhuria katika Mkutano huo
wanatoa shukrani kwa kupata Elimu hiyo ya Baishara na kuongeza kuwa sasa
watabadilika na kuchangamkia fursa zilizopo katika Migodi hiyo badala kulala
huku watu kutoka nje ya Mkoa wa Shinyanga wakifaidika
mwisho
picha namba
0056 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akifungua mafunzo ya
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga alioandaliwa Kampuni ya Barrick
Golg Mine.
picha
namba 0015-Meneja Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi Filbert Rweyemamu
akielezea faida za wafabiashara wa Shinyanga kufanya biashara na Migodi
ya Barrick.
picha namba 0042 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka mwezeshaji wa Kampuni ya Barrick.
picha namba 0049- baadhi ya Wafanyabiashara
walioshiriki katika Mkutano huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Ally Rufunga na Meneja Mgodi wa Buzwagi Filbert Rweyemamu.
No comments:
Post a Comment