Na Raymond Mihayo
Shinyanga
Febr 23, 2014.
BARRICK/ WAFANYABIASHARA.
KUENDESHA Biashara bila ya kufuata misingi ya
Sheria, taratibu na kiwango cha juu cha maadili ni moja kati ya Changamoto
zinazowakabili Wafanyabiashara Mkoani Shinyanga kupata fursa ya kufanya
biashara na Migodi ya Barrick Tanzania.
Hayo yalisemwa juzi na Afisa kutoka katika kitengo
cha Ugavi katika Migodi ya Afrikani Barrick gold Mine Dickson Liwumba katika
kikao kilichowajumuisha Wafanyabiashara waliopo Mkoani Shinyanga na wale
wanaofanya kazi na Migodi hiyo kutoka sehemu mbalimbali kanda ya ziwa.
Liwumba alisema kuwa mbali na Changamoto hiyo pia
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga wamekuwa hawapati fursa hizo pia kutokana
na bidhaa zao kutokuwa na kiwango na
kutomudu idadi ya vitu vinavyohitajika kwa wawekezaji hao.
Afisa huyo alisema kuwa pia ushirikiano baina ya
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga na kutoridhika pia katika suala zima la
kujiendeleza nalo ni tatizo kubwa hali ambayo inakuwa vigumu hata kuomba Zabuni
katika makapuni hayo pindi zinapotokea.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally
Rufunga akifungua mkutano huo uliandaliwa na Kampuni ya African Barrick Gold
Mine alisema kuwa Wafanyabiashara hasa wa Mkoa waShinyanga wanapaswa kujua kuwa
wao bado wana fursa kubwa ya kufanya kazi na migodi hiyo miwili.
Alisema kuwa anawashukuru pia Uongozi wa Migodi hiyo
miwili ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa kufanya mkutano na kutoa Elimu kwa
Wafanyabiashara hasa wa Mkoa wa Shinyanga katika kufuata Sheria na muda katika
kuendesha biashara zao hasa katika maeneo ya wawekezaji wa Migodi.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa
Wawekezaji wanataka bidhaa zenye kiwango na kuongeza kuwa kwa kutumia Mkutano
huo Wafanyabiashara wa Mkoa waShinyanga hawana budi kubadilika na kuongeza kuwa
kama kuna masuala ya kiserikali yanayowasumbua basi ofisi yake ipo wazi kwa
kutoa kutoa ushauri wa kibishara.
Pia Rufunga aliwaomba Kampuni hiyo kuwa na utaratibu
wa kuendesha mikutano kama hiyo mara kwa mara kwa lengo la kutoa Elimu kwa
Wafanyabiashara hao hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko hasa kwa
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga kuweza kuchangamkia fursa zilizopo katika
migodi inayowazunguka.
Mkutano huo wa siku moja uliofanyika mjini Shinyanga
ulijumuisha Wafanyabiashara kutoka Mkoa wa Shinyanga na wale ambao tayari
walishaanza kufanya biashara na kampuni hiyo huku lengo kubwa likiwa ni kutoa
Elimu kuhusu kuweza kupata fursa za kufanya biashara na Kampuni ya Barrick
mwisho
No comments:
Post a Comment