Na Raymond
Mihayo
Kahama
March 26, 2014.
WANANCHI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI
WATANZANIA wametakiwa kudumisha amani hapa Nchini ili waweze kufaidika na Matunda ya Serikali ya
Chama cha Mapinduzi ( CCM) katika utekelezaji wa Ilani yake kwa Wananchi hasa
katika sekta ya Maji kwa ujumla.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja aliyasema
hayo katika sherehe za kilele cha wiki ya maji iliyofanyika kimkoa katika
Kijiji cha Kagongwa WilayanI Kahama huku akisisitiza kuwa Chama cha mapinduzi
kipo pamoja na Wananchi wake katika kutekeleza ilani yake hasa katika sekta ya
maji.
Mgeja alisema kuwa Sekta ya maji ni moja kati sera
ya Chama cha Mapinduzi na kuongeza kuwa Chama hicho kitaendelea kuisimamia
Serikali katika kuhakikisha kuwa sera za Chama hicho zinatekelezwa ipasavyo kwa
Wananchi ikiwemo ile ya maji hasa katika maeneo ambayo huduma hiyo imekuwa
haipatikani.
“Chama cha Mapinduzi ndio jawabu ya majibu ya
matatizo ya Watanzania na sii kukimbilia chama kingine ambapo ni sawa na
kutokuwa na mwelekeo na majawabu ya majibu yenu hayawezi kupatikana”, Alisema
Khamis Mgeja Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliendelea
kusema kuwa kwa sasa malumbano kati ya
Wana CCM Mkoa wa Shinyanga kwa sasa hayana tija na badala yake wanachama
wa chama hicho waungane ili kuweza
kukiimarisha Chama hicho hali ambayo itaondoa migongano ndani ya chama hicho.
Aliendelea kusema kuwataka Wana CCM Mkoa wa Shinyanga
kuzungumzia maendeleo kwa sasa kwani Mkoa huo unajivunia kuwa Viwanda pamoja na
Rasilimali nyingi na kuongeza kuwa wanachama cha Mapinduzi wasisite kuzungumzia
maendeleo kwa kipindi hiki cha sasa.
Hata hivyo Mgeja aliwataka wananchi wa Mkoa wa
Shinyanga kuwa na imani na Chama cha Mapinduzi kwani kimewatoa mbali tangu
uhuru na ndio chama pekee inachoweza kutatua matatizo ya Watanzania pamoja na
kero za mbalimabali walizo nazo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally
Rufunga aliyekuwa Mgeni Rasmi katika sherehe alisema kuwa kwa mwaka huu
Serikali Mkoani Shinyanga imejitahidi kuondo kero za maji kwa Wananchi wake
lakini baadhi ya Wananchi wamekuwa wazito katika kuchangia gharama za maji
katika maeneo yao wanayoishi.
Rufunga alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo Serikali
imekwishatoa fedha kwa ajili ya miradi ya maji lakini Wananchi wamekuwa wazito
katika kuchangia gharama kidogo zinazotakiwa kutolewa kwa ajili ya kukamilisha
miradi hiyo.
mwisho
No comments:
Post a Comment