Na Raymond Mihayo
Kahama
Mrch 30, 2014.
WATANZANIA WATAKIWA KUTOACHAGUA KAZI ZA KUFANYA
WATANZANIA wakubwa
na Vijana wameshauriwa wasichague kazi za kufanya badala yake wafanye
kazi halali za kuwaingizia kipato na maslahi yao halali kuliko ya kufanya zile ambazo zipo juu
ya uwezo wao usiokuwa halali ambapo kwa sasa imekuwa kama ugonjwa mwingine unaolitafuna
taifa .
Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Shinyanga Khamis Mgeja wakati alipokuwa akikabidhi Msaada wa Luninga yenye
tahamani ya shilingi 260,000 kwenye kijiwe maarufu cha wajasiliamali cha Kahawa maarufu kwa jina la BBC katika mji
mdogo wa Isaka Wilayani Kahama.
Mgeja alitoa Msaada huo kutokana na ambi aliloombwa
na Wajasilimali wa kundi la BBC
alipofanya ziara ya kikazi ya chama ya kukagua shughuli za utekelezaji
wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi mwaka
katika Mji huo mdogo wa Isaka.
Wajasiliamali hao waliomba msaada huo wa Luninga ili
waweze kupata habari kupitia chombo hicho hasa nyakati za asubuhi na jioni
kabla ya kazi na baada ya kazi ili kwenda sambamba na mambo yanatokea ndani na
nje ya nchi.
Akipokea msaada huo wa Luninga kutoka kwa Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja, Mwenyekiti wa Wajasilimali hao wa BBC Ali
Salumu Msangi alishukuru na kuongeza kuwa msaada huo umefika katika kipindi
muafaka hasa wakati wa kipindi hiki cha Bunge la katiba linaloendelea Mjini
Dodoma.
Baada ya makabidhiano ya zawadi hiyo Mgeja aliwataka
wazee na vijana wajenge utamaduni wa kuridhika vipato vidogo wanavyovipata
kulingana na hali waliokuwa nayo badala ya kukimbilia vipato vya juu ambavyo
vipo nje ya uwezo wao wa kimataji.
Mgeja pia alisema kuwa hapa nchini bado kuna fursa mbalimbali ambazo
zinaweza kuwakwamua kiuchumi watanzania hususani Vijana na wale wa kawaida hasa katika sekta za Kilimo,
Uvuvi, ufugaji pamoja na uanzishwaji wa Viwanda vidogovidogo.
“Hapa nchini bado kuna fursa nyingi mbalimbali za kuinua uchumi kwa wananchi wa
kawaida hasa katika sekta za Kilimo, uvuvi, na hata ufugaji hali ambayo inaweza
kuleta mabadiliko kwa vijana wenye kipato kidogo”, Alisema Mwenyekiti huyo wa
Mkoa wa Shinyanga.
Mwisho
No comments:
Post a Comment