MWEZESHAJI WA SEMINA YA WANAHISA KUTOKA MAKAO MAKUU YA CRDB DAR ES
SALAAM MR NGELEJA MCHARO AKIENDELEA NA SEMINA HIYO ILIYOFANYIKA KATIKA
UKUMBI WA CARTAS MJINI KAHAMA.
IMEELEZWA kuwa Kutokuwepo kwa matumizi ya sarafu moja katika
soko la pamoja la Afrika Mashariki kumeleta athari kubwa zitokanazo na matumizi
makubwa ya fedha za kigeni katika nchi wanachama wa jumuia hizo.
Hayo yalieelezwa juzi na mwezeshaji
kutoka makao makuu ya bank ya CRDB Ngeleja Mcharo katika semina ya wana hisa wa
bank hiyo wilayani Kahama mkoani Shinyanga yenye lengo la kukuza uelewa wa soko la mitaji.
Mcharo alisema kuwa matumizi ya
fedha za kigeni katika soko la mitaji la afrika mashariki yameleta changamoto hususan
kwa wafanyabishara wanaofanya biashara katika nchi hizo.
Sambamba na hayo aliongeza kuwa uelewa
mdogo katika masuala ya soko la pamoja pia ni changamoto ikiwa ni pamoja na
baadhi ya sheria,kanuni,sera na vikwazo kutoondolewa katika muda uliopangwa.
Akizungumza kwa upande wa wafanyabiashara
wa Tanzania Mcharo alisema kuwa wanashindwa kuhimili ushindani wa soko la
pamoja kutokana na kutokuwa na mitaji mikubwa hali inayopelekea wafanyabishara wa
nje kushikilia soko hapa nchini.
Kwa upande wao washiriki wa semina
hiyo walisema kuwa semina za elimu ya hisa ziwepo mara kwa mara ili kuwajengea
uwezo zaidi wanahisa juu ya masuala ya kukuza mitaji .
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo
Joseph Manyala alisema kuwa vikao vingi vya benki ya CRDB vinafanyika jijini
Arusha hali inayofanya washiriki wengi kutoka sehemu za mbali kushindwa
kuhudhuria.
Awali akifungua semina hiyo meneja
wa benki ya CRDB tawi la Kahama Luther Mneney aliwataka wanahisa kuifanya benki
ya CRDB kama mali yao na kwamba wazidi kununua hisa kwa faida zao na bodi ndiyo
msimamizi.
Mneney alisema kuwa kwa sasa vijana
wengi hapa nchini hawataki kuju mambo ya kibenki kama ya kukuza mitaji au mambo
ya hisa halia ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na uelewa kuhusu mambo
ya kibenki.
“Vijana wengi wameshika mambo mengi
ambayo hayawasaidii katika maisha kama vile mambo ya mipira ya ulaya hali
ambayo inawafanya kupitwana wakati na mambo ya kibeki na watanzania msiwe makarai kwa mitaji ya watu wengine”,
Alisema Meneja huyo.
MATUKIO KATIKA PICHA:
WANAHISA WAKIWA KATIKA SEMINA
WANAHISA WAKISIKILIZA KWA MAKINI KATIKA SEMINA HIYO.
WADAU WA SOKO LA HISA WILAYANI KAHAMA WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO
WANAHISA WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO.
KATIBU MUHUTASI WA BENKI YA CRDB TAWI LA KAHAMA GRORY LAUWO KUSHOTO AKIWEKA KUMBUKUMBU YA SEMINA.
WANAHISA WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO.
MUWEZESHAJI AKIENDELEA KUTOA MAFUNZO
No comments:
Post a Comment