Thursday, April 10, 2014

MVUA YAHARIBU NYUMBA KIBAO HUKU KAYA 65 ZIKIKOSA SEHEMU YA KUISHI HUKO KABONDO KAHAMA


FAMILIA  zaidi 65 hazina mahali pa kuishi katika kijiji cha Kabondo kata ya Mwanase Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga baada ya nyumba zao  kusombwa na   Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kijiji hicho juzi na kusababisha hasara kubwa ya mali kwa wakazi hao.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kabondo Elias Paul alisema kuwa Mvua  hiyo iliyokuwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ilianza kunyesha majira ya saa nane za usiku na hivyo kusababisha maafa hayo makubwa.

Paul alisema kuwa mbali na uharibifu huo wa nyumba mvua hiyo pia imezoa mazao yalikuwa yamelimwa yakiwemo mpunga, na Wakulima katika kijiji hicho hali ambayo inafanya Wananchi hao wahitaji msaada wa haraka ili kuwanusuru tatizo na tatizo  la njaa linaweza kutokea kwa kipindi hiki.

Aidha Mtendaji huyo akiongea na Waandishi wa habari aliendelea kusema kuwa kutokakana na uharibifu huo mkubwa ambao pia umesababisha mazao kama yale ya Mpunga aliyokuwa shambani kwenda na maji hali ambayo inaweza kusababisha upungufu mkubwa chakula katika kata hiyo.

Hata hivyo Mtendaji huyo aliendelea kusema kuwa wananchi nyumba zao zilizochukuliwa na maji kwa sasa wamehifadhiwa na majirani zao huku wakisubiri msaada wowote kutoka katika ofisi ya ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama ili waweze kumudu maisha yao.

“Kwa sasa ndugu Mwaandishi wa habari hata usafiri wa kutoka katika kijiji hicho kuja mjini Kahama ni Mgumu kwani barabara hazipitiki unatumia muda wa masaa hata saba kutoka katika sehemu husika ambayo ni karibu kabisa na Mjini”, Alisema Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kabondo Aliasi Paul

Aidha aliendelea kusema kuwa msaada kama vile wa Mahema kwa wahanga hao unahitajika kwani kwa sasa sehemu walipojishikiza wamekuwa wakiishi zaidi ya watu 14 huku wengine wakikaa katika majiko ili kujisitiri wao na watoto.

“Kwa sasa wahanga hao katika sehemu walizojishikiza wanaishi zaidi ya watu 14 huku wengine wakiwa katika majiko ya kupikia hali ambayo inaweza kuleta kufumuka kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu”, Aliongeza Afisa Mtendaji huyo wa Kijiji cha Kabondo.

Katika Wilaya ya Kahama kuna uwezekano mkubwa wa wananchi kuendelea kuathirika na mvua za masika zinazoendelea kutokana na baadhi ya wananchi wengi hasa katika maeneo ya Vijijini kutokuwa na nyumba imara ambazo inaweza kuhilimi mvua hizo.


No comments:

Post a Comment