Wednesday, April 30, 2014

HABARI KUTOKA KAHAMA WIKI HII

Na Raymond Mihayo
Kahama
April 30, 2014.

MWALIMU AUWA MWANAFUNZI KAHAMA

MWANAFUNZI  mmoja mkazi  wa Jijini Mwanza Clinton Majembe ameuwawa kwa kupigwa na mama yake wa kambo Lupinda Kauli Mwalimu wa Shule ya Msingi Malunga mjini Kahama kwa kinachodaiwa kuwa kuwa mtoto huyo aliacha jiko jiko la gesi likiwa linawaka ndani.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Noel Mseven ambapo tukio hilo lilitokea usiku wa kuakia Ijumaa kuu alisema kuwa Marehemu alikuwa ni Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule moja mjini Bukoba.

Mseveni alisema kuwa Marehemu Clinton alikuja kumsalimia mama yake wakati wa likizo ndogo ya pasaka na hivyo kumkosa hali ambayo ilisababisha mama yake huyo wa kambo aliyekuwepo katika nyumba hiyo kupiga kutokana na kudai kuwa alikuwa amewasha jiko la gesi bila ya idhini yake.

Alisema kuwa Mama huyoa ambaye ni mtu wa matukio katika mtaa huo pia inasadikiwa pia aliwahi kmtishia mume wake kumuua na hivyo kusababisha kuukimbia mji wake mpaka kufikia hivi sasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Ernest Mangala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kwa sasa hayupo ofisi yupo nje kikazi na kuhaidi kulizunguzia tukio hilo pindi atakaporejea kazini hivi karibuni.

Mwisho.


Na Raymond Mihayo
Kahama
April 30, 2014.

ZIMAMOTO KAHAMA WAFANYIA KAZI MAKABURINI.

KATIKA hali ya kushangaza iliyojitokeza kwa Jeshi la Zimamoto la Halmashauri ya Mji wa Kahama ni pale ambapo wamekosa ofisi ya kufanyia kazi na kuhamishia katika eneo ambalo linasadikiwa kuwa lilikuwa na makaburi hapo awali.

Jeshi hilo ambalo ni muhimu katika matika matukio ya uzimaji wa moto katika Mji wa Kahama pia wamejikuta wakikosa ofisi za kufanyia kazi hali ambayo imewafanya kufanyia shughuli zao za kiofisi katika gari lao la kuzimia moto.

Baadhi ya watumishi wa Jeshi hilo wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuhsu kupatiwa eneo la kufanyia kazi lakini jitihada zao zimekuwa zikigonga mwamba bila ya mafanikio huku wakiendelea kusota katika mazingira magumu ya kufanyia kazi

Akiongea na Habarileo  juzi Mkaguzi wa Jeshi hilo Mkoa wa Shinyanga Rashidi Mwinyimkuu alisema kuwa madai hayo yanayodaiwa na Askari wa jeshi ni ya msingi na kungeza kuwa wamekuwa wakijitahidi kupata eneo la kufanyia kazi lakini mazungumzo bado yanaendeleo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala.

“Unajua ndugu Mwandishi Jeshi la zimamoto katika Halmashauri ya Mji wa Kahama limeanzishwa hivi karibuni baada ya kuzaliwa kwa Halmashari hiyo na kwa sasa tupo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha kuwa tunapata maeneo kwa ajili ya kufanyia kazi Ashari hawa”, Alisema Rashidi Mwinyimkuu.

Pia Mkaguzi huyo aliendelea kusema kuwa kwa sasa Wananchi wa Mji wa Kahama wanahitaji kupata elimu kubwa juu ya matukio yanayohusu moto ikiwa ni sambamba na kutumia vifaa maalumu vya kuzimia moto katika maeneo mbalimbali ya maduka mahotel na sehemu nyingine.

Aliendelea kusema kuwa Wilaya ya Kahama kwa sasa inakuwa kwa haraka zaidi na watu wakiendelea kujenga nyumba nyingi ikiwa ni pamoja na maeneo ya biashara kuwa mengi hali ambayo kwa kuwa na ofisi ya zimamoto katikati ya mji itasadia wa kiasi kikubwa kuwahi matukio.

Hata hivyo Mkaguzi huyo alisema kuwa Changamoto nyingine inayoikabili ofisi yake ya zimamoto ni pamoja na kutokuwa na namba maalumu kwa ajili ya Wananchi kupiga pindi matukio ya moto yanapotokea na kungeza kuwa hali hiyo inatokana na kutokuwa na ofisi maalumu kwa ajili ya kufanyia kazi.

Mwisho.


Na Raymond Mihayo
Kahama
April 30,2014.

TBL KUUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA MAUWAJI YA TEMBO

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imesema kuwa itaendelea kuungamkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupambana na winmbi la majangili wanaouwa Tembo hapa nchini hasa kwa kupitia bia yake ya Ndovu.

Hayo yalisemwa juzi na Afisa Tarafa ya Msalala Addy Mtaule wakati wa sherehe iliyoandaliwa na Kampuni hiyo ya bia iliyojumuisha wadau mbalimbali wa Kampuni hiyo na wauzaji wa bia katika mji wa Kahama kwa ujumla .

Mtaule aliyasema hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambaye alikuwa Mgeni Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo na kuongeza kuwa Serikali itakuwa bega kwa bega n a Kampuni hiyo

Alisema kuwa kwa sasa hapa nchini kumekuwa na wimbi kubwa la mauwaji ya Mnyama Tembo huku majangili hao wakichukua Pembe zake na kwenda kuuza katika nchi mbalimbali kwa lengo la kutafuta utajiri wa haraka.

Awali akitoa Salamu za TBL Meneja Mauzo kanda ya ziwa Sylivester Syzya alisema kuwa lengo kubwa la kufanya sherehe hiyo ni kufahamiana na kuongea mambo mbalimbali yanayohusu biashara hususani zile bidhaa zinazotengenezwa na Kampuni hiyo pamoja na wateja wao.

“Tuna muda mwingi hatujawakutanishja wateja wetu kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza kuhusu nini tufanye sisi kama Kampuni ya biasha na ni nini kimepungua ili tuweze kuboresha hasa katika bia ya Ndovu”, Alisema Syzya Meneja mauzo kanda ya ziwa.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa Kampuni hiyo itaendelea katika kuwajali Wateja wake katika mambo mbalimbali ya kuboresha biashara zao ili waweze kutimiza malengo yao la kuwa na mitaji mikubwa itakayowasadia katika kupanua wigo wa biashara.

mwisho

No comments:

Post a Comment