Monday, April 14, 2014

MWENYEKITI KAMATI YA MAAFA ALA FEDHA ZA RAMBIRAMBI ZA WAFIWA


 
Na Raymond Mihayo
Kahama
April 14, 14.

FEDHA ZA RAMBIRAMBI ZAWATOKEA PUANI MWENYEKITI NA KAMATI YAKE.

FEDHA zilizokuwa zimechangwa na waombezaji maarufu kama (Nzengo) katika msiba mmoja ulitokea katika kata ya Malunga Wilayani Kahama  zimezua tafrani baada ya waombezaji wa masiba kugundua kwa safu ya uongozi katika wa misiba walikuwa wakila fedha za Rambirambi za misiba inayotokea katika eneo hilo.

Hayo yalielezwa juzi na mmoja mkazi wa kata hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe baada ya viongozi hao wa misiba wakiongozwa na Mwenyekiti wao Ernest Soka kula fedha za rambirambi kiasi cha shilingi 120,000 zilizokuwa zimechangwa na wananchi hao kwa ajili ya msiba ulitokea tarehe 12/4/2014 katika kata hiyo.

Chanzo hicho habari kilisema kuwa mnamo siku hiyo ya msiba wa Kwanza jumla ya wahudhurianji katika tukio hilo walikuwa jumla ya watu 185 walioandikwa katika daftari za mahudhuri lakini wakati mwenyekiti huyo akitoa taarifa baada ya msiba kuwa kiasi gani kimepatikana kwa ajili ya kusaidia ndugu wa Marehemu ndio aliosema kuwa wahudhuriaji walikuwa  125 jambo ambalo sii kweli.

Alisema kuwa katika msiba wa pili ambao pia ulitokea katika siku inayofuata katika eneo hilo hilo wahudhuriaji wa msiba huo walikuwa 151 lakini cha ajabu alipunguza watu 11 kwa lengo la kujipatia fedha fedha yeye na Kamati yake ya msiba ya eneo hilo.

Aidha Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya kuwabana viongozi hao walikiri kuwa walikuwa wakila fedha hizo mara kwa mara wakati wa misiba hali ambayo wananchi wa eneo hilo waliamua kuitisha Mkutano ili kuwatenga viongozi hao kutokana na tabia hiyo mbaya walikuwa wakiifanya ya kula fedha zinachangiwa na wananchi hasa katika mambo ya maafa

Waliotuhumiwa kula fedha hizo za rambirambi ni Joshua Bavuma, Ernest Soka ambaye ndio mwenyekiti, Mwalimu Rwiza, Idd Mbarook pamoja mmoja aliyefamika kwa jina moja la Kapelo hali ambayo katika ya watu hao watano watatu walikubali kuzilipa fedha hizo kwa njia ya kuchangishana akiwemo mwenyekiti Ernest Soka, Kapelo pamoja Mwalimu Rwiza na kuongeza kuwa wengine wakuokaidi waliazimiwa kutengwa na jamii ya eneo hilo.

Hata Hivyo Mwenyekiti wa kamati ya maafa katika kata hiyo ya Malunga Ernest Soka alipohojiwa juu ya ubadhilifu wa fedha za rambirambi hizo alikana na kuongea kuwa watu katika eneo hilo wamekuwa na chuki pamoja na uroho wa mabaraka katika ngazi hiyo.

“Ndugu Mwandishi hayo ni maneno ya uzushi na chuki yaliopo katika mitaa yetu na sisi kutokana na tuhuma hizo hatujakubali kulipa feha hizo hata kidogo  hata hivi karibuni kuna mtu walizushia kuwa amefumaniwa na mke mtu jambo amblo sii la kweli nakushauri hayo mambo yaache na ninajua aliyekuja kumwambia mambo hayo ya uongo”, Alisema Ernest Soka Mwenyekiti wa kamati ya maafa

Mwisho.


No comments:

Post a Comment