Kahama
May 5, 2014.
MGEJA; KAULI YA LEMBELI CCM SIO MAMA YAKE NI
KUVIMBIWA MADARAKA
CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga kimesema kuwa
kauli ya Mbuge wa Jimbo la Kahama James Lembeli ya kusema kuwa Chama cha
Mapinduzi (CCM) sio mama yake ni kama kitendo cha kuvimbiwa Madaraka aliyokuwa
nayo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja
alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa Kata Isaka katika ziara yake ya
kuzungumzia maendeleo amani na Upendo na katika Wilaya ya Kahama pamoja na
kukagua shuguli za maendeleo kama ilani ya chama hicho inavyosema.
Mgeja alisema kuwa wao kama chama cha mapinduzi Mkoa
wa Shinyanga wamekuwa wakipokea simu mbalimbali kutoka kwa wadau kulaani
kitendo hicho kilichosemwa na Mbunge huyo tena mbele ya vyombo vya habari.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa Chama cha
Mapinduzi ndicho kimemfikisha Mbunge huyo hadi alipo na kimemfanya hadi kupata
fursa za kutembelea hadi nchi za nje lakini kwa kauli yakje hiyo aliyoisema
inakuwa aileti tija kwa chama hicho ambacho hadi hivi sasa ni Mbunge kupitia
CCM.
“Sisi hatuna taabu juu ya mambo mengine yanaymhusu
yeye kama kuunga mkono Serikali tatu lakini sisi kama Wananchama wa Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga tunapingana na kauli yake moja tu ya kusema Chama
cha Mapinduzi sio mama yake”,Alisema Khamis Mgeja Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Shinyanga.
“Leo katika Mkano huu sina nafasi ya kuzungumzia
kuhusu kauli ya Mbunge huyu kwani Katibu wa Itikadi na uenezi wa Mkoa
alishayasema haya hapo awali na kutuwakilisha uongozi wa Mkoa wa Shinyanga
katika kulaanui kitendo cha Mbunge huyo
tena wa CCM”, Aliongeza Khamis Mgeja.
Pamoja na Mambo mengine katika Mkutano huo Mgeja
aliwataka watanzania kuungano juu Serikali mbili katika mchakato wa kupata
katiba mpya mpya na kuwataka viongozi wa matawi ya CCM kuwaambia wananchi wao
juu faida za Serikali mbili badala ya kushabikia Serikali tatu kama walivyo
wabunge wa upinzani.
Pia Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga alisema
kuwa kitendo cha viongozi kupenda Serikali tatu ni kama mkitendo cha
kuwabebesha watanzani mzigo na kuongeza kuwa Serikali tatu ipo pamoja na
ukiunganisha Seriali za Mitaa lakini bado watanzania hawajajua hivyo.
Mwisho.
Kahama
May 5, 2014.
HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGA BAJETI ZA MICHEZO
CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga kimezitaka
Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kuwa zinatenga Bajeti za Michezo ambazo
zitawaendeleza vijana na kuwasadia kuachana na tabia ya kukaa vijiweni bila ya
kuwa na kazi ya za kufanya.
Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Shinyanga Khamis Mgeja wakati akiongea na viongozi wa Chama cha Mapinduzi
kuanzia ngazi ya mashina na mabalozi katika Mji mdogo wa Isaka na kuangalia
ilani ya chama hicho kama inatelezwa.
Mgeja alisema kuwa Sekta ya Michezo ni kama kazi
kama ilivyo kwa kazi zingine za kimaendfeleo na kuongeza kuwa sekta hiyo ni
ajira na inawasaidia Vijana kwa kiwango kikubwa katika kupambana na ugumu wa
ajira hapa nchini.
“Tunaweza kukuza
ajira kwa kutumia michezo na sisi kama Chjama cha map[induzi Mkoa wa
Shinyanga tunaziomba Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanfga kuhakikisha kuwa
zinaunga mkono na kusaidia vijana na katika sekta hiyo ya hichezo”, Alisema Mgeja
Mwenyekiti wa CC Mkoa wa Shinyanga.
Aidha Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa kwa
sasa Mkoa wa Shinyanga tumebahatika kupata Timu ya ligi kwa muda wa miaka
13 na kuongeza kuwa lazima tuiinge Mkono
timu yetu ya Stend United kwa sasa huku tukifanya jitihada za kuzipandisha timu
nyingine.
Kwa upande wake Mbuge wa Jimbo la Msalala Ezekiel
Maige aliyeambatana na Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa jumbo lake
limepania kuboresha sekta ya michezo hali ambayo itakuwa ni kama ajira kwa
Vijana wa jimbo hilo.
Maige ambaye alitoa kiasi cha shilingi milioni 1.4
kwa Vijana wa Kata ya Isaka kama kuunga Mkono katika kata hiyo alisema kuwa kwa
sasa yupo katika mazungumzo na baadhi ya wafandhili kwa nia ya kuhakikisha kuwa
Jimbo la Msalala linakuwa na timu katika kiwango cha juu.
Wakati huhuo Mbunge wa Jimbo la Kishapu Selemani
nchambi alihaidi kuchagia jumla ya mipira 28 ambayo itatumika katika mashindano
ya Msalala cup ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni hali ambayo itakuwa ni
chachu kwa viongozi wengine kuchangia katika sekya hiyo.
mwisho
Mbunge wa Joimbo la Kishapu Seleman Nchambi akiongoza maandamano katika Mji Mdogo wa Isaka
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Seleman Nchambi akiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakati wa maanadamano katika Mji wa Isaka
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akifungua ofisi ya Timu ya Mpoira wa miguu ya Iska Stars juzi
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Seleman Nchambi akitoa zawadi ya Vifaa ya kuuzia kahawa katika kijiwe cha BBC katika Mji mdogo wa Iska
hizo ni baadhi ya zawadi zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kishapu katika kijiwe cha Kahawa cha BBC Isaka juzi
Baadhi ya Viongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga wakionja Kahawa katika kijiwe cha BBC Isaka juzi.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Seleman Nchambi akifungua tawi la CCM katika kijiwe cha Kahawa cha BBC isaka juzi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiwa na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekieli Maige Muga Mfupi baada ya kufungua ofisi ya timu ya Isaka Stars juzi
No comments:
Post a Comment