Tuesday, May 6, 2014

SHINYANGA WALIA NA SERIKALI MBILI




Na
Kahama
Mei 6,2014

CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA SHINYANGA  CHAWATAKA WANANCHI KUWEKA MSIMAMO WA SERIKALI MBILI

CHAMA cha mapinduzi mkoani Shinyanga kimewataka wananchi kuweka msimamo wa kudai  serikali mbili katika mchakato wa kutafuta katiba mpya unaoendelea kujadiliwa katika Bunge na si serikali tatu kwani kufanya hivyo ni kama kuwaongezea Wananchi mzigo.


Wito huo umetolewa jana na mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakati akiwahutubia mamia ya watu katika kata ya Isaka kweye halmashauri ya Msalala wialayani hapa Mkoani  katika ziara yake ya kuhamasisha maendeleo katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Aidha Mgeja amewataka wananchi hao kuwadharau Wabunge  wanaobeza wenzao kwa maslahi yao nakuwataka wananchi hao wabaki namsimamo huo wa serikali mbili kwani kuwa na serikali tatu nikuongeza gharama ambazo hazina tija na kumpa Mwananchi mzigo.

“Nawaambieni kuwa kama mnataka Serikali tatu mpaka sasa zipo hizo Serikali yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na  zile Serikali za mitaa ambazo bado Watanzania hawajajua kama kuna kitu cha hivyo”, Alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja.

‘’Wazarauni wabunge wote ambao wanawabeza wabunge wetu wenye mapenzi mema na serikali yetu maana  wao wamo humo kwa lengo la kuvuruga wenzao  wamesahau kwamba huko mmewatuma ninyi wananchi na hawawatendei haki wanaanzisha mjina mengi mala UKAWA mala M4C  zimewasidia nini?.alisema Mgeja.

Aidha aliendelea kusema kuwa kuna baadhi ya Wabunge waliotoka bungeni wakipinga Serikali mbili na kuendelea kusema kama wameamua kufanya hivyo ni bora wakarudisha fedha za Wananchi ambazo walilipwa kama posho kwani huo ni wizi wa kuaminika.



Naye mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi aliwataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuachana na masuala ya ushabiki wa kisiasa na badala yake waangalie miradi ya maendeleo inayotekelezwa na chama cha Mapinduzi .

Nchambi alisema kuwa kwa sasa Watanzania lazima waelekeze macho yao katika shughuli za maendeleo na kuachana na watu wanabeza kuwa Chama cha Mapinduzi hakijawafanyia kitu Wananchi hali ambayo sii kweli

mwisho

No comments:

Post a Comment