Kyerwa BUKOBA
Juni 19, 2014.
MADINI YA BATI YATOROSHWA KWENDA RWANDA
WANANCHI wa
Wilaya mpya ya Kyerwa Mkoani Kagera wameiomba Serikali kudhibiti Madini ya Til
(Bati) yanayochimbwa katika Wilaya hiyo kutokana na baadhi ya Viongozi wa
Madini Mkoani hapa kushirikiana na Wanyarwanda katika kuyatorosha Madini hayo
kwenda nchi ya jirani ya Rwanda.
Wakiongea na Gazeti hili Wananchi hao walisema kuwa
wamekuwa wakishangazwa na wimbi la Watu hao kutoka katika nchi ya jirani ya
Rwanda kumimini katika mchimbo hayo kwa kudai kuwa hapa nchini hakuna soko wala
mitambo ya kusafishia madini hayo ya Bati.
Walisema kuwa sehemu hiyo maarufu kwa jina la
syndicate hapo siku za nyuma ilikuwa ikimiliwa na shirika la kutetea Wachimbaji
wadogowadogo (STAMICO) kwa sasa limevamiwa na Wanyarwanda na kujimilikisha
maeneo mbalimbali ya uchimbaji huku Watanzania wakinyimwa fursa hiyo na ofisi
ya Madini Mkoa.
Mmoja wa Wanyarwanda hao ambaye yupo katika machimbo
hayo tangu siku za nyuma Wabulungu Haruna alisema kuwa ofisi ya Madini Mkoa wa
Kagera imekuwa ikitoa Vibali vya uchimbaji wa Madini hayo ya Bati kwa
Wanyarwanda huku akisingizia kuwa hakuna
mtanzania anayeweza kufanya biashara hiyo kwani hapa nchini hakuna sehemu yenye
mitambo ya kusafishia madini hayo.
Haruna alisema kuwa Madini hayo ya bati katika eneo
hili yalikuwepo tangu siku za nyuma chini ya STAMICO lakini baada ya shirika
hilo kujitoa ndipo Wanyarwanda hao walipoamia katika Kijiji hicho na kusingizia
kuwa soko kubwa la Madini ya Bati lipo katika nchi ya Rwanda na sii Tanzania na
hivyo kuwafanya wazawa kubaki kuwa madalali tuu.
“Tunaomba ofisi za uhamiaji Mkoa wa Kagera kuja
katika eneo hilo kwani Wanyarwanda ni wengi sana wanaokuja kufanya biashara hii
huku ikisemekana kuwa hawana vibali vya kuishi na vya kufanya Biashara hiyo ya
madini hayo hapa nchini”, Alisema Wabulungu Haruna mchimbaji wa eneo hilo.
Kwa upande wake Afisa Madini Mkoa wa Kagera
Arbogasti Kalist alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya Suala hilo alisema kuwa
kweli Madini ya Bati yapo katika eneo hilo lakini hakuna mtanzania yeyote
liyejitokeza katika kuomba kibali cha kufanya shughuli za uchimbaji katika
maeneo hayo.
“Pia ndugu Mwandishi Watanzania katika madini hayo
waanatumika kama Madalali tuu kwa kuwa hapa nchini hakuna mitambo ya kuchenjua
madini hayo na hivyo hali ambayo Wanyarwanda wana mashine hizo na kufanya
biashara hiyo kuendeshwa na Wanyarwanda kutoka nchi ya jirani”, Alisema Afisa
Madini huyo.
Pia alisema kuwa kuwa kuhusu majengo hayo ya
Serikali kupangishwa Wanayarwanda Afisa Madini huyo alisema kuwa baada ya
Kampuni ya Stamico kuondoka waliona kuwa majengo hayo yasibaki wazi na hivyo
kuamua kuyapangisha Wananchi walipo katika eneo hilo wakiwemo Wanyarwanda hao.
Katika suala la Risiti Afisa huyo alisema kuwa
waliingia mkataba na Kijiji kwa lengo la kugawana mapato yanayotokana na ushuru
wa wachimbaji huku stakabdhi hizi feki zikiwa na mihuri inayooesha imegongwa
kutoka katika ofisi za Madini za Mkoa.
mwisho
No comments:
Post a Comment