Wednesday, June 11, 2014

MSAFARA WA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI ANNA TIBAIJUKA LAPATA AJALI

 GARI ALILOKUWA AKISAFIRIA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI ANNA TIBAJIUKA LIKIWA KATIKA KITUO CHA POLISI KAHAMA MUDA MFUPI BAADA YA KUPATA AJALI
 GARI HILO KAMA LINAVYOONEKANA KWA MBELE
 LIKIWA KATIKA KITUO CHA POLISI MJINI KAHAMA
GARI HILO AINA YA TOYOTA LANDCRUSER V8






Kahama
Juni 11, 2014.

WAZIRI TIBAIJUKA ANUSURIKA KIFO.

WAZIRI wa  Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi  Anna Tibaijuka juzi alinusurika kifo baada ya gari aliyokuwa akisafirika kutoka Bukoba kwenda Dodoma kupata ajali  kwa kugonga Punda katika Kijiji cha Wen dele Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11.7 za jioni likijumuisha gari namba STK 5857 alilokuwa akisafiria Waziri huyo akiwa na familia yake mali ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendele ya makazi lililokuwa likiendeshwa na dereva Linusi Eliasi (42).

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenye alisema kuwa Waziri Tibaijuka alikuwa na baadhi ya wanafamilia wake waliokuwa wakitoka Bukoba kwenda Dodoma kwa ajili ya kuwahi shughuli za Bunge zinazoendelea.

Kaimu Kamanda huyo alisema kuwa baada ya kufika katika eneo hilo alikatisha Punda katikati ya Barabara na katika harakati za Dereva kumkwepa ndipo gari hilo lilipomgonga na kisha mnyama huyo kufa papo hapo.

Kihenya alisema kuwa katika ajali hiyo hakuna mtu aliyeumia ila kuna baadhi ya watu waliopata majeraha madogo madogo ikiwa ni pamoja na Waziri huyo aliyepata mstuko kidogo lakini baadaye hali yake iliendelea vizuri.

Hata hivyo hivyo msafara huo wa Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi Anna Tibaijuka ulilala mjini Kahama na jana asubuhi ulipatiwa usafiri mwingine kutoka katika uongozi wa Wilaya kwa ajili ya kuwapeleka Mjini Dodoma kuwahi vikao vya Bunge.

Pia katika hali ya mshangao wa watu waliomiminika katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa ajili ya kumjulia hali mama huyo na kumpa pole lakini Waziri huyo na msafara wake walikuwa wakipatiwa matibabu na wauguzi katika Hotel moja iliyopo pembeni mwa Hospitali ya Wilaya.

mwisho


No comments:

Post a Comment