VIONGOZI wa
Siasa na Wale wa Madhehebu ya Dini hapa nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele
katika suala zima la kuhubiri amani katika Mikutano yao na sehemu za ibada ili
watanzania waweze kujua umuhimu wa kjuwa na utulivu hapa nchini.
Hayo yalisemwa juzi na Alfred Mtaule aliyekuwa Mgeni
Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya katika warsha ya siku
moja iliyoandaliwa na shirika lisilo la Kiserikali la Search for Common Ground
kupitia mradi wake wa Amani.
Mtaule alisema kuwa kwa kuwatymia viongozi wa Siasa
pomoja na wale Dini suala la Elimu juu ya amani linaweza kuwafikia jamii ya
watu wengi kwani wao ndio wanaokuwa nao kwa wingi zaidi kuliko watu wa aina
yeyote ile.
“Kuwa kiongozi wa siasa au wa dini ina maana ni
kuielimisha jamii ili iweze kuelewa kwa kundi kubwa kwa pamoja na hali hiyi
itafanya wanatanzania wengi kuelewa juu ya suala zima la kudumisha amani tulio
nayo”, Alisema Mtaule
Alisema kuwa kukiwa na amani mambo mengi yanaweza
kufanyika ikiwa ni pamoja na watu kufanya shughuli zao bila ya kuwa na wasiwasi
wowote hasa jamii iliyopo katika sehemu zenye migodi ambapo mara nyingi huwa na
migogoro isiyomalizika.
Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Search for
Common Ground Jacob Mulikuza kutoka tawi la Tarime alisema kuwa lengo la
shirika lake ni kutoa Elimu kwa wananchi walipo kandokando ya Migodi ya dhahabu
ya dhahabu inayomilikiwa na Kampuni ya
Barrick.
Mulikuza alisema kuwa Warsha hizo kupitia mradi wa
amani wanaziendesha katika Migodi ya Barrick Buzwagi, Barrick Bulyanhulu,
Barrick Tulawaka pamoja na Mgodi wa Barrick North Mara ikiwa ni kuwaweka Wakazi
wa kando ya mgodi kuwa karibu na wawekezaji hao.
Aidha aliendelea kusema kuwa shirika hilo limeona
kubuni mradi huo kutokana na Sehemu nyingi zenye rasilimali zinaonekana kuwa na
kutoelewana baina ya wawekezaji wa maeneo hayo pamoja na watu wanaoishi
pembezoni kwa wawekezaji hao hususani wale wa migodi.
Warsha hiyo iliwajumisha viongozi mbalimbali kutoka
katika madhehebu ya Dini, Watendaji wa kata wa sehemu za uchimbaji wa madini,
Maafisa maendeleo ya jamii, Maafisa kutoka katika Migodi ya Barrick Buzwagi na
Bulyanhulu pamoja na watu wa kada mbalimbali walishiriki katika kuchangia mada
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment