Sunday, April 13, 2014

MASHINDANO YA MPESYA CUP YAANZA KUTIMUA VUMBI KAHAMA


 Maandamano ya kuelekea katika uwanja wa Taifa Mjini Kahama yaliojumuisha Timu 26 tayari kwa ufunguzi wa mashindano ya Mapesya Cup
 Mkuu wa Wilaya ya Kahama  benson Mpesya akisamiana na Wachezaji wa Timu ya Ngaya FC katika uzinduzi wa mashindani ya Mpesya CUP yalionza juzi Wilayani Kahama
 Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akifungua mashindani ya Mpesya Cup yatakayosaidia kupata Timu ya Wilaya ya Kahama
 Baadhi ya Tumu zilizshirikia katika maandamano ya ufunguzi wa mashindano ya Mpesya CUP
 Wachezaji wa Timu mbalimbali wakiwa katika maandamno
 Mwenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja nae alikuwa mmoja kati ya Viongozi walishiriki katika maandamano hayo

 Mkuu wa Wilaya Kahama Benson Mpesya na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakiwa katika maandamano


SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imesema kuwa haitawatupa Vijana hasa katika masuala mazima ya michezo kwa lengo la kuinua uchumi wa Wilayani hii sambamba na kupata timu itakayoshiriki ligi kuu kwa miaka ya mbele.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mpesya aliyasema hayo wakati akifungua mashindani ya Mpira wa miguu maarufu kama Mpesya cup ambayo yanashirikisha jumla ya timu 26 za Wilaya ya Kahama.

Mpesya alisema kuwa haiwezekani Wilaya ya Kahama pamoja na kuwa rasilimali nyingi ikiwemo wawekezaji katika sekta za migodi na Tumbaku wapo lakini Wilayah ii inakosa timu inayishiriki ligi kuu hapa nchini.

Aidha alisema kuwa lengo la mashindano ya Mpesya cup ni kukuza vipaji kwa Vijana wa Wilaya ya Kahama sambamba na kutafuta wachezaji ambao wataunda timu ya kombaini ya Wilaya ya Kahama ambayo itashiriki katika mashindano mbalimbali.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama aliendelea kusema kuwa mpira ni starehe  na inakuza akili  na kungeza kuwa kwa sasa pia ni ajira hali ambayo itawafanya wachezaji kufanya michezo kama sehemu yao ya kujipatia kipato.

“ Kwa sasa tumedharia Wilaya ya Kahama lazima tupate timu itakayocheza ligi kuu kwa hali tunayo na Rasilimali tunazo na wachezaji tumieni michezo katika katika kuonyesha viapaji vipaji vyenu ulionavyo”, Alisema Mkuu wa Wilaya ya kahama Benson Mpesya.

Pia aliwataka wachezaji kutumia michezo kama sehemu ya kujenga urafiki  na mahusiano mazuri na kutoa onyo kwa waamuzi mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanachezesha michezo hiyo kwa kufuata sheria 17 za soka.

Katika michezo hiyo hiyo ya Mpesya cup mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na seti moja ya jezi, kikombe  na mpira mmoja wakati wa pili atapa kiasi cha shilingi 500,000 pamoja na seti moja ya jezi na mpira .

Michuano hiyo tayari imeanza juzi kwa mechi moja katika timu ya Ngaya FC na Ambassador na kumalizika kwa matokeo ya timu ya Ambassador kuinfunga timu ya Ngaya FC kwa jumla ya mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment